HabariMilele FmSwahili

Oparesheni dhidi ya washambulizi katika hoteli ya Dusit yakamilika

Awamu ya kwanza ya oparesheni dhidi ya washambuliaji katika hoteli ya Dusit D2 mtaani Westlands hapa Nairobi imekamilika. Waziri wa usalama wa kitaifa Dkt Fred Matiangi amesema kilichosalia ni maafisa wa idara ya jinai kuanzisha uchunguzi wao kuhusiana na shambulio hilo. Matiangi amesema kuwa eneo hilo litasalia kufungwa ili kuruhusu uchunguzi.

Amewapongeza maafisa wa usalama walioweza kudhibiti washambuliaji. Hata hivyo dkt Matiangi hajadhibitisha idadi kamili ya washambuliaji wakiwa wangapi. Kadhalika Matiangi amewahakikishia wakenya usalama wao akiwataka kuendelea na shughuli za kawaida. Amesema kenya iko imara kukabili tishio lolote la utovu wa usalama.

Naye katibu mkuu wa shirika la msalaba mwekundu Abbas Gullet amewatetea maafisa wa usalama dhidi ya madai ya kutotoa taarifa kabambe wakati wa oparesheni hiyo anayosema iliendeshwa kwa mpangilio mwafaka.

Show More

Related Articles