HabariMilele FmSwahili

Watu 14 wamedhibitishwa kuuwawa katika shambulizi la Dusit D2

Watu 14 wamedhibitishwa kuuwawa na wengine wengi kujeruhiwa. Akitangaza hayo rais Uhuru Kenyatta pia amedhibitisha kuwa magaidi wote waliotekeleza shambulizi hilo wameuwawa na maafisa wa usalama.

Rais Kenyatta amewapongeza maafisa wa usalama kwa namna walivyoshughulikia shambulizi hilo akisema ni ishara ya Kenya kuwa tayari kuwadhibiti maadui wanaoivamia. Kulingana na rais walinda usalama wamefanikiwa kuwaokoa watu zaidi 700

Vile vile rais amesema licha ya uwekezaji uliowekwa katika sekta ya usalama nchini serikali imetambua haja ya kuongeza juhudi katika kudhibiti tishio la ugaidi. Amesema serikali itawasaka na kuhakikisha wahusika wote wa shambulizi hilo wananaswa na kuchukuliwa hatua.

Show More

Related Articles