Mediamax Network Limited

Watu 174 Wameokolewa Kutoka Kwenye Shambulizi La Kigaidi Eneo La Riverside.

Zaidi ya watu 174 wameokolewa salama na maafisa wa usalama usiku wa kuamkia leo kutoka majengo yalioko eneo la Riverside jijini Nairobi.

Yakijiri hayo Waziri wa usalama wa ndani ‘Fred Matiang’I anasema asasi za usalama pia zimefanikiwa kuthibiti hali ya usalama katika majengo yote yalioko eneo hilo kuliko tokea shambulizi la kigaidi mapema jana jioni.

Hata hivyo waziri wa usalama hakutoa maelezo yoyote kuhusu idadi ya waliojeruhiwa au kuuawa wakati wa shambulizi la jana katika mkahawa wa Dusit D2 jijini Nairobi.

Kulinagana na Matiang’I vikosi vya usalama vingali vinaendeleza uchunguzi eneo la tukio huku usalama ukiwa umeimarishwa katika maeneo yote nchini.