K24 TvNEWSSwahiliVideos

SIASA ZA UKAMBANI ZACHUKUA MWELEKEO MPYA

Mkutano wa Jumatano iliyopita katika eneo la Matuu kaunti ya Machakos uliowahusisha magavana wote watatu wa Ukambani uliashiria kwamba mambo si shwari katika siasa za Ukambani.

Magavana hao Charity Ngilu, Dkt. Alfred Mutua na Profesa Kivutha Kibwana walionekana kumsuta kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka kwa kumtaja kikwazo kwa maendeleo na anayelenga kuhujumu utendakazi wao.

Show More

Related Articles