HabariPilipili FmPilipili FM News

Twalib Mbarak Kuingia Rasmi Afisini Leo.

Afisa mkuu mpya wa tume ya kukabiliana na ufisadi EACC Twalib Abdallah Mbarak atachukuwa rasmi hatamu za uongozi hivi leo katika taarifa EACC imedhibitisha kuondoka afisini Halake Waqo aliyekamilisha muhula wake wa miaka 6 jana.

Twalib aidha atakuwa anaapishwa Jumatatu ijayo mbele ya jaji mkuu David Maraga.

Mbarak aliyeidhinishwa na kamati ya bunge ya masuala ya kisheria mwezi uliopita aliapa kuhakikisha kuwa kesi za ufisadi zinachunguzwa upesi na washukiwa wote kufunguliwa mashtaka.

Show More

Related Articles