HabariPilipili FmPilipili FM News

Wizara Ya Elimu Kukagua Mfumo Wa NEMIS.

Shughuli ya kuwasajili wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza inakamiliam leo.

Imechukua Juma zima kwa zoezi hilo kutekelezwa kufuatia agizo la waziri wa elimu Balozi Amina Mohamed.

Aidha ni usajili uliotekelezwa kiteknologia kupitia kwa mfumo wa NEMIS.

Wizara ya elimu inatarajiwa kukagua mfumo wa NEMIS kubaini iwapo ulifanikisha usajili wa asilimia 100 ya wanafunzi waliojiunga na kidato cha kwanza.

Show More

Related Articles