HabariMilele FmSwahili

Watu 20 walazwa baada ya kula nyama inayodaiwa kuharibika kaunti ya Bomet

Watu 20 wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya Longisa, kaunti ya Bomet baada ya kula nyama iliyoharibika. Waathiriwa walikimbizwa hospitali baada ya kuanza kutapika na kulalamikia maumivu ya tumbo. Aidha walikula nyama hiyo katika  hafla ya mazishi kwenye kijiji cha Tabok, Bomet ya kati. Afisa wa afya eneo hilo Phillip Ruto amebaini kuwa maafisa wa afya wametumwa katika kijiji hicho kuanzisha uchunguzi. Ruto ameongeza kuwa uchuuzi wa vyakula umepigwa marufuku kufuatia tukio hilo.

Show More

Related Articles