HabariMilele FmSwahili

Gavana Sonko atarajiwa kutaja anayempendekeza kuwa naibu gavana wake leo

Gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko leo anatarajiwa kutaja anayempendekeza kuwa naibu gavana wake. Miongoni mwa wanaopigiwa upato kutwaa wadhifa wa naibu gavana ni askofu Margaret Wanjiru, mwanaharakati Agnes Kagure, wakili Karen Nyamu na Jane Weru. Nairobi imekuwa bila naibu gavana tangu Januari mwaka jana wakati Polycarp Igathe  alijiuzulu kadhalika sonko anatarazamiwa leo kumchagua mrithi wa Janet Ouko aliyekuwa waziri wa elimu kaunti hii.

Gavana Sonko pia amedokeza azma ya kulifanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri kwa lengo la kukabili ufisadi.

Show More

Related Articles