HabariPilipili FmPilipili FM News

Usimamizi Wa Hospitali Ya Wilaya Ya Malindi Walalamikia Vibanda Vilivyoizunguka Hospitali Hiyo.

Wasimamizi wa hospitali ya wilaya ya Malindi wamehimiza wakuu wa kuthibiti usafi eneo hilo kuingilia kati na kuviondoa vibanda vyote vilivyokaribu na lango la hospitali hiyo.

Wakizungumza na waandishi wa habari wakuu hao wamesema vibanda hivyo vimekuwa vikificha wahalifu na pia kuzindisha uchafu ambao huathiri wagonjwa kwenye hospitali hiyo.

Kwa upande wao maafisa wanaothibiti usafi eneo hilo wamesema wanatafuta njia mbadala ya kuwahifadhi wafanyibiashara hao ambao hutegemea vibanda hivyo kufanyia biashara zao.

 

Show More

Related Articles