HabariPilipili FmPilipili FM News

Baadhi Ya Shule Mombasa Hazijapata Vitabu Vya Mtaala Mpya.

Imebainika kwamba kufikia sasa kaunti ya Mombasa bado haijapokea vitabu vya mfumo mpya kama walivyoahidiwa na wizara ya elimu .

Haya ni baada ya waziri wa elimu Amina Mohamed kuafikia kuwa vitabu hivyo vitaweza  kufika katika shule zote za umma wiki hii.

Baadhi ya walimu wakuu tuliozungumza nao, wameitaka wizara ya elimu kuhakikisha vitabu hivyo vinafika kwa haraka ili waweze kuvitumia kama muongozo.

Johnstone Kimbuga na David Mulei ni walimu wakuu wa shule ya msingi ya Khadija na Shimo la tewa hapa Mombasa.

Show More

Related Articles