HabariMilele FmSwahili

KEPSA yataka wakenya kuchangamkia vita dhidi ya Ufisadi

Wito umetolewa kwa wadau katika sekta mbali mbali na wakenya kwa ujumla kushiriki kikamilifu katika vita dhidi ya ufisadi nchini. Naibu mwenyekiti wa wakfu wa wafanyibiashara katika sekta ya kibinafsi KEPSA Patrick Obath anasema jinamizi la ufisadi limekuwa likichangia kenya kupoteza shilingi trilioni 1 kila mwaka. Amewataka wakenya kukoma kulaumi asasi na maafisa waliotwikwa wajibu wa kukabili uovu huo badala yake akiwataka kujitwika wajibu wa kuumaliza. Obath amedokeza kuwa wakfu wa KEPSA utaandaa kongamano la kitaifa kuhusu vita dhidi ya ufisadi baadaye mwezi huu kujadili tatizo hilo.

Show More

Related Articles