HabariPilipili FmPilipili FM News

Wazazi Taita Taveta Wahimizwa Kujukumikia Watoto Wao Kikamilifu.

Wito umetolewa kwa wazazi katika kaunti ya Taita Taveta kutia juhudi kuwatimizia watoto wao mahitaji ya kimsingi bila kukwepa pamoja na kuunga mkono juhudi za serikali kama njia mojawapo ya kuboresha sekta ya elimu.

Wito huu umetolewa na gavana wa kaunti hiyo Granton Samboja alipozindua mpango wa  serikali ya kaunti hiyo kufadhili  wanafunzi 100 katika shule za upili watakaojiunga na kidato cha kwanza mwaka huu.

Wakati huo huo Samboja amewataka wazazi kuhakikisha wanachukua jukumu la kuwafunza wanao tabia njema kupitia ushauri nasaha  pamoja na kushirikiana na walimu huku akiwaonya wanaetendendekeza watoto wao kuwa watakuwa wanachangia kutofaulu kwao.

Samboja aidha amekashifu hatua ya wizara ya elimu nchini kupitia kwa tume ya uajiri waalimu kubagua jamii za kaunti yake wakati wa uajiri licha ya kuwepo idadi kubwa ya waalimu walio na tajriba inayohitajika.

Show More

Related Articles