Swahili Videos

Gavana Sonko akemea ufisadi wa fedha za karo

Gavana wa Nairobi Mike Sonko amejitokeza bila kupepesa macho, na kusisitiza kuwa ataendelea vivyo hivyo na njia yake ya kutawala, hadi ahakikishe amepambana na wafisadi kwenye kaunti.

Sonko, ameyasema haya jijini Nairobi, siku moja baada ya aliye kuwa waziri wa elimu Janet Ouko, kudai kuwa Sonko, aanajaribu  kumharibia jina kwa tuhuma za ufisadi.

Aidha, Sonko ametangaza atafanya mabadiliko ya mawaziri wake ifikiapo Ijumaa.

Show More

Related Articles