HabariPilipili FmPilipili FM News

Visa Vya Utapia Mlo Kwale Vyatajwa Kupungua.

Wizara ya afya kaunti ya Kwale  imethibitisha  kupungua  kwa asilimia 50 ya maradhi yanayosababishwa  na ukosefu wa lishe bora miongoni mwa wakaazi  wa eneo la Kinango  kutokana  na kuimarika  kwa kilimo   kinachoendelezwa kando kando  mwa bwawa la mwache.

Afisaa wa kitengo  cha lishe  katika hospitali ya Kinango  daktari  Brian Muasya  amesema ujenzi wa bwawa la Nyalani umepelekea  jumla ya familia 400 kugeukia ukulima kupitia unyunyiziaji wa maji wa mimea yao shambani hata licha ya makali  ya  kiangazi  kushuhudiwa  katika eneo hilo   .

Ujenzi wa  bwawa la Nyalani huko  Kinango kaunti ya Kwale  kwa kima cha shilingi milioni 200   ulitekelezwa  kwa ufadhili wa wakfu wa mpesa  , shirika la msalaba mwekundu ,serikali ya kitaifa  na ile ya kaunti.

Show More

Related Articles