HabariPilipili FmPilipili FM News

Washukiwa Wawili Wakanusha Mashtaka Ya Udanganyifu Mahakamani Mombasa.

Watu wawili wamefikishwa katika mahakama ya Mombasa hii leo kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo kwa maafisa wa polisi.

Saida Abdulrahman na mumewe Mohammed Abdulrahman wamefikishwa mbele ya Jaji wa mahakama kuu ya mombasa Christine Ogweno, wakikabiliwa na tuhuma za kutoa habari ya uwongo kwa polisi, ambapo mnamo mwezi septemba mwaka jana wa 2018 ilidaiwa saida Abdurahman alitekwa nyara akiwa na uja uzito wa miezi minane. Badae uchunguzi wa polisi na madakitari ulibaini kuwa saida hakuwa mja mzito, na kwamba hakuwa na uwezo wa kupata mimba.

Wawili hao hata hivyo wamekana mashtaka dhidi yao na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi elfu mia moja wote wawili.

Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 24 ya mwezi huu wa Januari.

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

 

Show More

Related Articles