HabariPilipili FmPilipili FM News

Msishirikiane Na Matapeli, Serikali Yahimizwa.

Serikali imetakiwa kutofanya kazi na washikadau wa sekta ya matatu ambao ni matapeli.

Kulingana na shirikisho la usafiri wa umma lililojumuisha wenyekiti na wkaurugenzi wa wamiliki wa matatu na vyama vya sacco, mwenyekiti wa chama cha wenye matatu Simon Kimutai pamoja na washirika wake hawajali maslahi ya wenye matatu nchini wakisema wanapigania maslahi yao.

Wanasema wakuu hao wangekuwa mstari wa mbele kupigania kutoondolewa kwa matatu kuhudumu katikati mwa jiji badala yake wameunga mkono hatua hiyo.

Wakati huo huo wametaka kuelezwa ni lini mafunzo ya BRT yaani Bus RAPID Transit yaliendelezwa bila ya wao kufahamishwa.

Show More

Related Articles