HabariPilipili FmPilipili FM News

Rais Kenyatta Awaonya Wanasiasa Wanaoeneza Siasa Za Chuki.

Rais Uhuru Kenyatta amewaonya wanasiasa dhidi ya kueneza siasa za chuki na mgawanyiko.

Badala yake rais amewarai viongozi kuungana pamoja kuwahudumia wakenya katika pembe zote za taifa hili.

Aidha kiongozi wa nchi amesisitiza kuwa ataendelea kufanya kazi na viongozi kutoka mirengo yote ya kisiasa, na hasa kinara wa ODM Raila Odinga kuona kuwa maisha ya wakenya wote yanaboreshwa kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo.

Show More

Related Articles