HabariPilipili FmPilipili FM News

Serikali Yapiga Marufuku Disco Matanga Kilifi.

Disco Matanga katika kaunti ya Kilifi zimepigwa marufuku kuendelea kupita saa tano za usiku.

Waziri wa usalama wa ndani Fred Matiang’i amewataka maafisa wa usalama kuhakikisha hakuna disco matanga itakayoendelea baada ya masaa yaliyotengwa.

Matiang’i pia amekashfu kisa cha chifu wa lokesheni ya Shariani David Kahindi aliyevamiwa na vijana baada ya kusitisha disco matanga katika eneo hilo.

Aidha Matiang’i amewataka maafisa wa polisi kuhakikisha vijana wote waliomshambulia chifu huyo wanatiwa nguvuni.

Show More

Related Articles