HabariK24 TvSwahiliVideos

KIDATO CHA KWANZA : Wanafunzi wapya waripoti shuleni

NEMIS

Shughuli ya usajili wa wanafunzi katika kidato cha kwanza ilianza rasmi kote nchini hii leo huku kila shule ikilazimika kutumia mfumo wa kupitia mtandao wa NEMIS kuwasajili wanafunzi.

Hata hivyo baadhi ya wazazi ambao walitaka uhamisho kutoka shule moja hadi nyingine walihangaika pale majina ya watoto wao yalikosekana kwenye mtandao huo wa NEMIS katika shule walizodhani walikuwa wamepata nafasi.

Huku haya yakijiri, serikali imezindua rasmi shughuli ya usambazaji vitabu vya mtaala mpya kwa shule zote za msingi nchini.

 

Show More

Related Articles