HabariPilipili FmPilipili FM News

Baadhi Ya Wanafunzi Wanaojiunga Na Kidato Cha Kwanza Kutojumuishwa Kwenye Mfumo Wa Kidijitali.

Wanafunzi wa kidato cha kwanza ambao watapata barua zao za  shule moja kwa moja kutoka kwa walimu wakuu hawatajumuishwa kwenye mfumo wa kidijitali wa serikali wa kusajili wanafunzi wa NEMIS.

Hayo ni kulingana na waziri wa elimu balozi Amina Mohamed.

Waziri Amina amewaonya walimu wakuu dhidi ya kutoa barua za kusajili wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa wazazi wanaotembelea shule zao kutafutia watoto wao nafasi.

Amina aidha anasema wanafunzi ambao watakosa kusajiliwa kwenye mfumo wa serikali wa NEMIS hawatakua na rekodi yoyote ya kuonyesha kuwa walijiunga na shule za upili. Kauli ya Amina imetiliwa mkazo na katibu katika Wizara ya Elimu Belio Kipsang.

Show More

Related Articles