HabariPilipili FmPilipili FM News

Mhalifu Sugu Auliwa Mombasa.

Maafisa wa polisi wameeleza kumpiga risasi mtu mmoja anayeaminika kuwa miongoni mwa wahalifu sugu ambao wamekuwa wakitatiza wananchi eneo la Fire Mwembe Tayari mjini Mombasa.

Akithibitisha tukio hilo kamanda wa polisi kaunti ya Mombasa Johnstone Ipara anasema jambazi huyo alikuwa miongoni mwa wenzake wanne, na kwamba alipigwa risasi na kuuawa alipo jaribu kumshambulia afisa wa polisi kwa kisu , wakati polisi wakishika doria eneo hilo usiku wa kuamkia leo.

Ipara anasema polisi watasalia imara kuona kuwa wakazi wa mombasa wako salama, akiahidi kuwakabili vikali wahalifu wanaotatiza usalama wa wananchi.

 

 

Show More

Related Articles