HabariPilipili FmPilipili FM News

Kaunti Ya Mombasa Yashtumiwa Kwa Kuwatenga Walemavu.

Serikali ya Kaunti ya Mombasa inaendelea kushutumiwa kwa kutowajumuisha watu wenye ulemavu katika mipango yake ya maendeleo.

Mwanaharati wa kutetea masuala ya wenye ulemavu katika Shirika la Vision For the Blind Mkalla Shanga anaeleza kusikitishwa na jinsi ambavyo licha Sheria kutoa fursa ya kuwa na wawakilishi wawili kwenye bunge la Kaunti hadi kufikia sasa wadhfa huo umepewa mtu mmoja pekee.

Hata hivyo Mkurugenzi wa Shirika la kutetea haki za watu wenye ulamavu linalojulikana kama Pamoja Tunaweza, Ruth Awinja ameonekana kutofautiana na kauli yake Mkalla Shanga.

Show More

Related Articles