HabariPilipili FmPilipili FM News

Wazee Wakimijikenda Wamegadhbishwa Na Hatua Ya Polisi Ya Kutibua Mkutano Wao.

Wazee wa jamii ya kimijikenda eneo la Maweni Likoni hapa mombasa wameeleza kugadhabishwa na hatua ya polisi kuutibua mkutano waliopanga kuufanya eneo hilo licha ya kuwa na vibali vyote hitajika

Katibu wa Baraza hilo Ali Mwasirima na Diwani wa Bofu Ahmed Salama wamesema hatua hiyo ni kinyume cha sheria na tishio kwa wazee hao katika kuisaidia serikali kukabiliana na makundi ya uhalifu yanayohangaisha wakaazi.

OCS wa kituo cha inuka patrick Lumumba aliyetoa kibali Cha mkutano huo amesema alilazimika kuukatiza kwa hofu ya kiusalama .

Show More

Related Articles