HabariMilele FmSwahili

Mwili wa mwanafunzi David Maina anayedaiwa kuuwawa na polisi Nairobi kufanyiwa upasuaji

Mwili wa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Leeds anayaedaiwa kuuwawa kwa kupigwa risasi na afisa wa polisi mtaani Kibra, Nairobi unafanyiwa upasuaji hii leo kubaini chanzo cha kifo chake. Carilton David Maina aliuwawa katika eneo la laini saba usiku wa ijumaa wiki iliyopita. Baadhi ya  wanaharakati wa kutetea haki za kibinadamu wanatarajiwa kuandamana leo kushinikiza haki kwa mwanafunzi huyo cariln david maina. Tayari mamlaka ya ipoa imeanzisha uchunguzi kuhusu mauaji hayo huku idara ya polisi ikiapa kumchukulia hatua afisa atakayepatikana na hatia.

Show More

Related Articles