HabariMilele FmSwahili

Kesi ya kupinga ushindi wa gavana Mutua yatupilia mbali

Gavana wa Machakos dkt Alfred Mutua amepata afueni baada ya mahakama ya juu kuidhinisha ushindi wake katika uchaguzi mkuu wa 2017. Majaji wa mahakama hiyo wakiongozwa na jaji mkuu David Maraga wametupilia mbali kesi iliyowasiolishwa na Wavinya Ndeti na kushikilia kuwa uchgauzi wa Mutua ulikuwa wa haki. Naye gavana wa kwale Salim Mvurya ana kila sababu ya kutabasamu baada ya mahakama ya juu kuamua kuwa uchaguzi wake ulikuwa wa haki. Kesi hiyo iliwasilishwa na wapiga kura Suleiman Mwamlole Warrakah, Mwarapayo Mohamed wa-mwachai  na matsudzo hamisi mwamrezi. Wakati huo huo majaji hao wametupilia mbali ushindi wa mbunge wa Ugenya Chris Karan. Tume ya IEBC imeagizwa kuandaa uchaguzi mpya wa ubunge eneo hilo.

Show More

Related Articles