HabariPilipili FmPilipili FM News

Walimu Watangaza Tarehe Rasmi Ya Mgomo.

Walimu wametangaza kuitisha mgomo wa kitaifa kuanzia Januari mbili mwaka ujao wa 2019.

Akizungumza mapema leo katibu mkuu wa chama cha walimu KNUT Wilson Sossion ameituhumu tume ya kuajiri walimu nchini TSC , kwa kuendelea kuwahamisha walimu wakuu wa shule za msingi na upili kinyume na makubaliano yao na tume hiyo ya mwaka wa 2017.

Sossion amekashifu uhamisho wa hivi punde wa zaidi ya walimu wakuu 3000 akiutaja kuvunja na kuhangaisha familia za walimu, huku akiitaka tume ya TSC kubatilisha uhamisho huo mara moja.

Kauli yake imeungwa mkono na mwenyekiti wa kitaifa wa chama cha walimu nchini KNUT Wyclif Omucheyi.

Haya yanajiri wakati ikiwa imesalia wiki mbili shule kufunguliwa kwa muhula wa kwanza januari.

 

Show More

Related Articles