HabariMilele FmSwahili

Mahakama yamruhusu Jackson Kibor kumpa mkewe wa zaidi ya miaka 43 talaka

Mahakama ya Eldoret imemruhusu mkulima na mfanyibiashara maarufu kaunti ya Uasin Gishu Jackson Kibor  kumpa talaka mkewe wa 3 Naomi Jeptoo. Kibor ameishi na Jeptoo kwa zaidi ya miaka 43.Ni uamuzi uliootolewa na hakimu naomi Wairimu  baada ya kubaini kuwa mkulima huyo alikuwa akidhulumiwa na mwanamke husika. Kupitia wakili wake stanley kagunza Kibor anasema yuko tayari kumpa mgao wake wa mali japo anasema ardhi hatapata.

Mwaka  jana mwezi Oktoba mahakama  ya  Eldoret ilikubalia  ombi lingine la  mkulima Kibor kumtaliki  mkewe wa pili Josephine Kibor waliyeishi naye kwenye ndoa miaka 53 sababu kuu za talaka  hizo  zikiwa ukosefu mapenzi ndani ya ndoa na pia kudhulumiwa na wake  hao.

Show More

Related Articles