HabariMilele FmSwahili

Wenyeji Komarock waendelea kukadiria hasara kufuatia ubomoaji unaoendelea mtaa huo

Askari wa kaunti wakati huu wanaendeleza ubomozi wa majumba ya makaazi eneo la Nyama Villa mtaani Kayole hapa Nairobi. Ubomozi huu ulioanza mapema leo, umewaathiri zaidi ya wakaazi elfu 3 waliokuwa wakiishi katika kipande cha ekari 29 mtaani humo. Kulingana na wenyeji, hawakupewa notisi ya ubomozi huo na kuituhumu serikali ya kaunti kwa kuharibu mali zao

Zaidi ya polisi 50 wametumwa kushika doria wakati wa ubomozi kufuatia kisa cha mshikeshike kilichoibuka baina ya polisi na  wenyeji mapema leo. Awali mbunge wa Embakasi Kusini Benjamin Gathiru alijipataa taabani alipokamatwa alipojaribu kutatiza ubomozi husika. Ubomozi huu unawadia baada ya mfanyabiashara mmoja hapa njini kushinda kesi mahakamani hapo jana ilipoamuriwa kwamba ndiye mmiliki halisi wa ardhi hiyo

Show More

Related Articles