HabariPilipili FmPilipili FM News

NTSA Yataka Mtaala Wa Mafunzo Ya Udereva Ufanyiwe Marekebisho.

Washikadau katika sekta ya usafiri wanasema ipo haja ya mtaala wa mafunzo ya udereva kufanyiwa marekebisho wakiulaumu kwa kukosa kujitosheleza.

Washikadau hao wanasema madereva nchini wanafaa kupitia masomo ya kujihusisha mbali na hali ya sasa ambapo wanazingatia elimu ya vitabu.

Aidha wamesema kushirikisha maoni ya wengi katika kubadlisha mtaala wa mafunzo ya udereva kutasaidia kupunguza ajali nchini.

Akiwajibu waliohudhuria kikao hicho cha kutafuta suluhu kwa ajali za barabarani kilichifanyika hapa Mombasa Mkurugenzi mkuu wa NTSA Francis Meja ameahidi kuleta mwafaka kwa tatizo hilo.

 

Show More

Related Articles