HabariPilipili FmPilipili FM News

Mwenyekiti Wa Chama Cha Maendeleo Ya Wanawake Kilifi Yuko Kwenye Hatari Ya Kutimuliwa Uongozini.

Mchakato wa kumfurusha mwenyekiti wa chama cha maendeleo ya kinamama Kaunti ya Kilifi Witness Tsuma kutoka kwenye uongozi sasa umeanza kupigwa jeki na baadhi ya viongozi katika Kaunti hio.

Hatua hii inajiri baada ya kuzuka malalamishi kuhusian na ubadhirifu wa  pesa za maendeleo ya kina mama hao huku pia wakidai tangu kuasisiwa kwa serikali za ugatuzi hajawahi kuitisha mkutano ili kuelezea mwelekeo wa chama hicho sawia na kukwepa mikutano ya chama hicho.

Seneta maalum wa Kaunti ya Kilifi Christine Zawadi amesema kutojitokeza kwa mwenyekiti huyo katika mikutano ya maendeleo ndio kumechangia pakubwa kuzorota kwa chama hio.

Kwa upande wake aliyekuwa Seneta maalum Kaunti ya Mombasa Emma Mbura amesema tayari wameanza mchakato wa kufuatilia utumizi wa pesa za kinamama hao huku akiongeza kuwa hatua hio imechangia pia kuporwa kwa raslima za chama hicho.

Show More

Related Articles