HabariMilele FmSwahili

Wauguzi Bomet watangaza kusitisha mgomo wao

Wauguzi kwenye vituo vya umma kaunti ya Bomet wamesitisha mgomo wao uliodumu wiki moja. Katibu wao Vincent Rono anasema wamechukua hatua hiyo baada ya serikali ya kaunti kuonyesha nia ya kuzungumza nao.Akiwahutubia wanahabari, amewasihi wauguzi kurejea kazini na kuwahudumia wenyeji kwa bidii. Rono aidha amewataka wawakilishi wadi kupitisha bajeti ya ziada kwa ajili ya nyongeza ya mishahara huku akiongeza kuwa hawatasita kurejelea mgomo endapo mazungumzo yatafeli.

Show More

Related Articles