HabariMilele FmSwahili

Bunge kuandaa mkao spesheli kuidhinisha uteuzi wa Twalib Mbarak kama afisa mkuu mtendaji wa EACC

Bunge la kitaifa leo linaandaa mkao spesheli ambapo wabunge watakuwa wanaidhinisha au kupuzilia mbali uteuzi wa Twalib Mbarik kuwa afisa mkuu mtendaji wa tume ya ufisadi EACC. Mbarak Ijumaa lililopita aliezea hari aliyonayo kusaidia taifa kukabili jinamizi la ufisadi. Mbele ya kamati ya bunge kuhusu haki na sheria, Twalib alielezea jinsi amejiandaa kuharakisha kesi zinazofungamana na ufisadi kwa kuwasilisha ushahidi madhubuti kuwezesha wafisadi kukabiliwa. Iwapo Twalib ataidhinishwa na bunge atatwaa wadhifa ambao umekuwa ukishikiliwa na Halake Waqo ambaye amehdumu afisini humo kwa miaka 6 sasa.

Show More

Related Articles