Pilipili FmPilipili FM News

Tayari Super Cup Yanoga Samburu.

Mbunge wa Kinango Benjamin Tayari amewahimiza vijana kuhakikisha kuwa wanajiepusha na utumizi wa mihadarati ili kuendeleza talanta zao.

Akiongea wakati wa fainali ya kipute cha tayari super cup eneo la Samburu mbunge huyo ameendelea kusistiza kuwa vijana wana nafasi kubwa sana katika jamii ikiwa watazidi kuendekeza vipaji vyao vya soka.

Mbunge huyo ameanzisha ligi wakati huu wa likizo ili kuwaleta vijana pamoja na kuwaepusha na uhalifu na utumiaji wa dawa za kulevya.

Ligi hio inajumuisha timu 167 na inachezwa kwa mfumo wa muondoano kwa kila wadi ambapo Jumapili kulichezwa fainali katika wadi ya Samburu -Chengoni na timu iliyoibuka washindi ni Lions Fc ambayo iliicharaza Ghaibu Fc kwa mabao mawili kwa moja.

Benjamin Tayari alifurahishwa na vipaji vya soka kwenye fainali hio na kuahidi kuunda timu ambayo itaiwakilisha Kinango katika mashindano mbali mbali kwenye soka.

Washindi katika mechi hizo alijishindia jezi, kikombe pamoja na pesa taslimu.

Mechi za ligi hio zitaendelea wiki hii kwenye wado za Puma na  Macknon.

Show More

Related Articles