Mediamax Network Limited

Mbunge Mwadime Akinzana Na Rais Kenyatta Kuhusu Uteuzi Wa Bodi Ya Madini.

Mbunge wa Mwatate Andrew Mwadime amesuta uteuzi wa bodi ya madini uliofanywa na rais Uhuru Kenyatta na kusema kuwa haukuwa na mwakilishi kutoka jamii ambapo madini hutoka kwa wingi.

Akiongea kwenye mkutano na wakaazi kwenye shule ya msingi ya Mwatate , Mwadime amesema kaunti ya Taita Taveta ndiyo  inaongoza kwa wingi wa madini nchini na licha ya hilo hakuna mkaazi aliyeteuliwa kwa bodi hiyo.

Kadhalika ametoa wito kwa serikali ya kaunti ya Taita Taveta kuzingatia ahadi yake ya kuwanunulia vifaa wachimbaji madini hasa wasio na uwezo mkubwa wa kifedha ili kuwawezesha kutekeleza shughuli yao bila kutatizika.