Mediamax Network Limited

Matokeo Ya KCSE Kutangazwa Wiki Hii.

Matokeo ya mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne KCSE yanatarajiwa kutangazwa wakati wowote wiki hii.

Kulingana na duru kutoka wizara ya elimu, zoezi la kusahihisha mtihani huo lilikamilika ijumaa wiki iliyopita.

Waziri wa elimu Amina Mohammed alisema matokeo ya KCSE mwaka huu yatatangazwa mapema kabla ya tarehe 20 desemba.

Zaidi ya wanafunzi elfu 600 walifanya KCSE mwaka huu.