Swahili Videos

Madereva walevi kuwindwa usiku na mchana

Inspekta jenerali wa polisi Joseph Boinnet ametoa onyo kali dhidi ya madereva wanaoendesha gari wakiwa walevi, huku akisema kwamba maafisa wa trafiki sasa watanza kufanya uchunguzi wa kupima ulevi mchana na wala siyo usiku pekee.
Boinnet aliyasema hayo huku akithibitisha kwamba ikilinganishwa na mwaka jana idadi ya ajali za barabarani imepungua kwa asilimia 50, huku akisema kwamba idadi ya maafisa wa polisi wa trafiki itaongezwa.

Show More

Related Articles