HabariMilele FmSwahili

Boinnet awatahadharisha madereva walevi msimu huu wa krismasi

Inspeta generali wa polisi Joseph Boinnet amewatahadharisha  madereva walevi msimu huu wa krismasi kwamba watakutana na kifaa cha kupima viwango vya pombe mwilini maarufu alcoblow asubuhi, tofauti na ambavyo oapresheni hizo zimekuwa zikiendeshwa usiku. Boinnet amewatahadharisha madereva walevi kwamba chuma chao ki motoni. Lengo anasema ni kuzuia ajali za barabara.

Alikuwa akizungumza katika hafla ya kuwatuza maafisa 25 kutoka vitengo mbali mbali vya idara ya polisi katika afisi yake jijini Nairobi. Tuzo hizo zilizotolewa na mfanyibiashara mashuhuri Manu Chandaria ambaye amedokeza kwamba wakfu wake unajenga kituo cha kuwasaidia waathiriwa wa ajali za barabarani.

Show More

Related Articles