HabariMilele FmSwahili

Twalib ahojiwa kujaza nafasi ya afisa mkuu mtendaji wa EACC

Twalib Abdalla Mbarak, anasema ana uwezo wa kushikilia wadhfa wa afisa mkuu mtendaji wa tume ya kupambana na ufisadi. Akizungumza alipofika mbele ya kamati ya bunge la taifa kuhusu uteuzi, amesema atatoa mapendekezo mapya ya jinsi ya kupambana na ufisadi ili kufanikisha vita hivyo. Amesema iwapo atateuliwa ataomba bunge kuweka sheria mwafaka ambazo zitafanikisha kutwaliwa mali za umma kutoka kwa wafisadi, kwani ilivyo kwa sasa kuna changamoto nyingi kisheria kutwaa mali hizo.

Ameongeza tajriba na maadili yake yanamweka katika nafasi bora ya kuhuudmu kwenye tume hiyo muhimu katika vita dhidi ya ufisadi. Twalib aliibuka wa kwanza kati ya watu 13 waliowasilisha maombi ya kujaza nafasi hiyo.

Show More

Related Articles