HabariMilele FmSwahili

Mpango wa afya bora kwa wote waanza katika hospitali za Nyeri, Kisumu,Machakos na Isiolo

Mpango wa afya bora kwa wote yaani UHC umeanza kwa mpigo hospitali za kaunti za Nyeri, Kisumu, Machakos na Isiolo zikifurika wagonjwa leo. Hii baada ya Rais Uhuru Kenyatta jana kuzindua huduma za afya chini ya uhc ambazo zinapokelewa bila malipo. Katika kaunti ya Nyeri, hospitali ya rufaa, mamia ya wagonjwa wamefika kupokea huduma mbali mbali za afya, wengi wakipongeza jinsi wanavyoshughulikiwa

Hali ni sawia kaunti ya Kisumu ambapo, wagonjwa wamepongeza serikali kwa jitihada zao kuhakikisha huduma nafuu zinakaribishwa.

Show More

Related Articles