HabariPilipili FmPilipili FM News

Mbunge Owen Baya Ahimiza Serikali Ya Kilifi Kupiga Jeki Uvuvi.

Mbunge wa Kilifi Kaskazini  Owen Baya amelitaka bunge la kaunti ya Kilifi  kupitisha mswada unaolenga kuwafaidi wavuvi na vyombo vya kisasa wakati wa kutekeleza shughuli zao za kivuvi.

Anesema kutowezeshwa kwa wavuvi hao na vyombo vya kisasa kumewasababishia kuvua samaki wachache mno ikilinganishwa na wavuvi wenzao kutoka   maeneo ya Pemba na Zanzibar ambao hutumia vifaa vinavyowawezesha kuvua maji makuu.

Akizungumza mjini Kilifi Baya anasema hatua hio imechangia pakubwa kwa wavuvi wengi katika kanda ya Pwani kusalia katika lindi la umaskini  licha ya kwamba bahari hindi kuwa moja wapo ya raslimali zinazoweza toa mchango mkubwa wa uchumi wa Pwani.

Show More

Related Articles