HabariMilele FmSwahili

Walimu wapinga makato ya kuchangia mpango wa makaazi

Walimu wamepinga makato yanayonuia kuchangia mpango wa serikali wa makaazi.  Wakionyesha gadhabu zao, walimu wamemzomea katibu katika wizara ya nyumba Charles Hinga alipokuwa akitoa maelezo kuhusu mpango huo wa serikali, kwenye kongamano la walimu wa chama cha KNUT hapa Nairobi. Wanatuhumu serikali kwa kukosa kushauriana nao kabla ya kupendekeza makato hayo ya asilimia 1.5 kwa wafanyikazi wa serikali.

Makato haya mapya yanapaswa kuanza kutekelezwa Januari mwakani kwa wafanyikazi wote wa serikali

Show More

Related Articles