HabariMilele FmSwahili

Serikali ya kaunti ya Nairobi yaanza ubomozi wa hoteli ya Grand Manor mtaani Gigiri

Serikali ya kaunti ya Nairobi wakati huu inaendesha ubomozi wa hoteli ya kifahari ya Grand Manor. Haya yanajiri siku moja baada ya mahakama kuidhinisha ubomozi wa hoteli hiyo kwa misingi kuwa ni tishio kwa usalama wa makao makuu ya shirika la Umoja wa Ulaya mtaani Gigiri. Utata kuhusiana na hoteli hiyo uliibuka mwezi Agosti mwaka huu baada ya mmiliki wake Praful Kumar kukamatwa na maafisa wa tume ya kukabili ufisadi EACC huko Kilifi kwa tuhuma za kujaribu kumhonga gavana wa Nairobi Mike Sonko ili azuie unomozi wake.

Show More

Related Articles