HabariPilipili FmPilipili FM News

Mwashetani Awataka Maafisa Wa Usalama Lungalunga Kukoma Kuwahangaisha Wahudumu Wa Bodaboda.

Mbunge wa Lungalunga Khatib Mwashetani  amemtaka  kamishna  wa  kaunti ya Kwale  Karuku Ngumo  kutoa agizo  kwa  maafisa wa usalama hususan wa eneo la Lungalunga  kukomesha tabia za  kuwahangaisha na kuwapiga wahudumu wa bodaboda kwa madai kuwa wanaendesha shughuli zao kinyume cha sheria .

Akizungumza  katika sherehe za maadhimisho ya siku ya jamhuri  zilizofanyika katika shule ya msingi ya lungalunga ,Mwashetani amekiri kuwepo  kwa wahudumu wa bodaboda ambao hawana vibali , japo kuitaka idara ya usalama  kuwapatia muda wa kujitafutia riziki akisema kuwa afisi yake tayari inashughulikia vibali vya wahudumu hao.

Ni kauli iliyoungwa mkono na mwakilishi wa wadi ya Mwereni Manza Beja na Yule wa wadi ya  Dzombo Patrick Mangale.

Show More

Related Articles