HabariPilipili FmPilipili FM News

Rais Kenyatta Atoa Onyo Kali Kwa Wafisadi.

Rais Kenyatta amekariri kuwa sheria haitamsaza yeyote mwenye azma ya kupalilia ufisadi nchini.

Kenyatta amesema hatakubali fedha za wanachi kukwamilia kwenye mifuko ya watu wachache.

Amesifia kuanzishwa kwa mbinu ya huduma mashinani kuwa itasaidia kudhibiti ufisadi.

Amekemea vikali afisi za serikali zinazowahangaisha wakenya katika kupata huduma kuwa sheria itafuata mkondo wake.

Amewarai wanachi kuwa mstari wa mbele kuripoti visa vyovyote vya ufisadi ili kuisaidia serikali kuudhibiti.

Aidha rais Kenyatta ametahadharisha idara za mahakama dhidi ya kuendeleza ufisadi na kulemaza haki.

Kiongozi wa nchi amesema ipo haja ya vitengo vya  serikali kuzingatia haki.

Rais ameyasema hayo kwenye maadhimisho ya 55 ya sherehe za Jamhuri jijini Nairobi.

Show More

Related Articles