Pilipili FmPilipili FM News

Aliyekua Naibu Gavana Wa Kaunti Ya Kilifi Kenneth Kamto Ameuawa.

Aliyekuwa naibu gavana wa kaunti ya Kilifi Keneth Kamto ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana nyumbani kwake Nyali hapa Mombasa alfajiri ya leo.

Haya yamethibitishwa na kamishna wa kaunti ya Mombasa Evans Achoki.

Kwa sasa mwili wa marehemu unahifadhiwa katika hifadhi ya maiti katika hospitali ya Pandya.

Chanzo cha mauji hayo bado hakijabainika.

Show More

Related Articles