People Daily

Usalama Wazidi Kudorora Kisauni.

Wakaazi wa Kisauni katika kaunti ya Mombasa wanalalamikia ukosefu wa usalama katika maeneo hayo wakitaja magenge ya ujambazi yamekuwa yakitekeleza mauaji ya mara kwa mara Jambo ambalo limeibua hofu miongoni mwao.

Wakaazi Hawa wamelimbikizia lawama vitengo vya usalama kwa madai ya kukosa kufika katika matukio kwa wakati na pia kushirikiana na magenge haya katika kutekeleza uhalifu.

Licha ya kuwepo kwa vitengo vya walinda usalama katika maeneo hayo , wakaazi hao wametaka wazee wa mitaa na wale wa nyumba kumi kushika Doria ili kupigana na wahalifu wanaoishi miongoni mwa wananchi.

Haya ni baada ya watu watatu wanaohofiwa kuwa miongoni kwa genge linalowahangaisha wakaazi hao kutiwa mbaroni na maafisa wa polisi

Show More

Related Articles