HabariMilele FmSwahili

Maafisa 5 wa serikali ya Sudan wafariki kwenye ajali ya helikopta

Gavana na maafisa wasiopungua sita wa serikali ya Sudan katika jimbo la Al-Qadharif wamefariki katika ajali ya helikopta iliyotokea katika jimbo hilo lililoko mashariki mwa nchi kwenye mpaka wa pamoja wa nchi hiyo na Ethiopia. Mashuhuda wamevieleza vyombo vya habari kuwa, helikopta hiyo iliripuka baada ya kugonga mnara wa mawasiliano wakati ilipojaribu kutua katika jimbo la Al-Qadharif. Taarifa rasmi ya serikali haijatolewa kueleza sababu hasa ya ajali hiyo.B Bila kutoa maelezo zaidi, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti kuwa watu kadhaa pia wamepelekwa hospitalini kwa ajil ya kupatiwa matibabu.Gavana wa jimbo la Al-Qadharif, Mirghani Saleh, mkuu wa serikali yake, mkuu wa polisi wa jimbo hilo pamoja na waziri wa kilimo ni miongoni mwa waliofariki katika ajali hiyo.

Show More

Related Articles