K24 TvNEWSSwahiliVideos

Wafanyakazi 10 wa NHIF na KPC, wazuiliwa Muthaiga

Aliyekuwa afisa mkuu mtendaji wa shirika la Bima ya Afya ya Kitaifa (NHIF), Geoffrey Mwangi, hatimaye amejisalimisha katika afisi za Idara ya Upelelezi Jumapili.

Hii ni baada ya afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma, kuagiza yeye pamoja na maafisa wengine wa NHIF, pamoja na wengine kutoka Shirika ya Mafuta Nchini (KPC), kujisalimisha kujibu mashtaka ya kuhusika katika ufisadi katika nyadhifa walizo nazo.

Maafisa hao ambao ni zaidi ya 10  wamezuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Muthaiga wakisubiri kuwasilishwa katika Mahakama Kuu ya Milimani hapo kesho.

Show More

Related Articles