Swahili Videos

Raila awasuta wabunge kuhusu mishahara

Naibu wa rais william ruto sasa anawataka  wafanyikazi wa serikali kutekeleza majukumu yao kikamilifu bila wasi wasi wowote, akitaja kuwa vita dhidi ya ufisadi vitawakumba tu wale wanaohusika na ufisadi huku akiwakosoa vikali wanaoingiza siasa kwenye masuala ya vita dhidi ya ufisadi.
Haya yanajiri huku kinara wa Odm Raila Odinga akiwataka wabunge wasioridhika na mshahara wanaolipwa kujiuzulu nyadhifa zao.
Akizungumza huko Kisumu mapema hii leo, Raila anakariri kwamba visingizo  wanavyotumia baadhi ya wabunge kujipatia nyongeza ya mishahara havina msingi na vinakwenda kinyume na katiba.

Show More

Related Articles