Swahili Videos

Maafisa 10 wa KPC na NHIF wakamatwa

Makachero kutoka idara ya upelelezi wa jinai wamewatia mbaroni wasimamizi wakuu wa shirika la kenya pipeline kufuatia madai ya ufisadi katika shirika hilo.
Miongoni mwa waliotiwa mbaroni ni mkurugenzi mkuu  Joe Sang, katibu wa shirika Gloria Khafafa na Vincent Cheruiyot ambaye ni meneja mkuu wa uagizaji bidhaa.
Aidha maafisa wengine kutoka hazina ya kitaifa ya matibabu-NHIF- pia wamewatiwa mbaroni, kufuatia madai hayo hayo ya ufisadi huku maafisa zaidi wakitarajiwa kukakamatwa.

Show More

Related Articles